Mazishi
ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na
watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha
Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika
katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza
katika manispaa ya Shinyanga.
Mwanafunzi huyo
aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo
kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha
kutobolewa Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha
Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi.
Akizungumza wakati wa
mazishi ya mwili wa marehemu yaliyofanyika LEO MCHANA naibu meya wa
manispaa ya Shinyanga David Nkulila alilaani kitendo cha kinyama
alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la
polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.
“Kifo cha mtoto huyu
ni mapenzi ya mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la
hili lifuatiliwe hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo
vya ukatili dhidi ya watoto vinatishia amani Shinyanga”,alieleza
Nkulila.
Kwa upande wake
Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige alisema suala la ulinzi kwa
watoto ni jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo
kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili
vinavyoendelea mkoani Shinyanga.
Naye mwenyekiti wa
mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo yalikofanyika mazishi ya mtoto huyo
bwana Peter Juma Kitundu alisema kifo cha mtoto huyo kinatia simanzi
kubwa kwani kimesababishwa na binadamu huku akiiomba serikali kulifanyia
uchunguzi wa kina tukio hilo na lisiingizwe suala la siasa.
Kwa upande wake
mwinjilisti Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi
alilaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii
kumrudia mwenyezi mungu kwa kuondokana na matendo mabaya.
No comments:
Post a Comment