ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, August 18, 2014

WATU NANE WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA MWL.NYERERE WAKIINGIA NCHINI KWA PASPOTI BANDIA ZA MATAIFA TOFAUTI YA ULAYA


 Idara ya Uhamiaji Nchini, imewakamata Raia wa nane (8) wa kigeni wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Nyerere, wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya Ulaya. Wageni hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini tarehe 15.08.2014 majira ya saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la Ndege la Uturuki yenye Namba TK 603,  wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa Raia wa Sweden na Belgium.


  Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.      

kukamatwa kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji haramu nchini ambapo suala  la Udhibiti wa Mipaka linapewa kipaumbele. akizungumzia tukio hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji zinafuatwa. "Idara ya Uhamiaji, iko macho hatulali kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila mtu awe Raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"    .

   Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri kurudishwa walikotoka.  Hili ni wimbi lililoibuka hivi karibuni kwa baadhi ya Raia wa nchi za Iraq, Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea Mataifa ya Ulaya.

Majina ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye mabano ni kama ifuatavyo;



1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT    -  SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)

3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE    - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF   - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI    - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI      - IRAQ, PPT. NO. G 1111623 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...