Aliyekuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Fred Mpendazoe.
Na Mwandishi wetu
Aliyekuwa
mgombea wa ubunge katika Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA), Fred Mpendazoe amejitokeza kuwania nafasi ya Makamu mwenyekiti wa chama hicho.
Mpendazoe
ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Kishapu kupitia CCM kabla ya kujiuzulu
wadhifa huo na kujiunga na Chadema ametangaza msimamo wake akisema kuwa
atasimamia ajenda zifuatazo kuhakikisha Chadema inachukua dola 2015
Mkakati
wa kwanza amesema akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti ataimarisha
Chadema kama taasisi, akisema kuwa mfumo uliopo sasa haujawa imara hasa
sehemu za msingi na matawi.
Alifafanua
kuwa wanananchi wengi hujitokeza kwenye mikutano ya hadharal akini
inakuwa vigumu kuwafuata ili kuwapatia elimu ya uraia
Hivyo
akiwa Makamu Mwenyekiti atashawishi vikao vya maamuzi kama kamati kuu
kutenga rasilimali za kutosha kwenda kuimarisha misingi, matawi na ofisi
za majimbo na mikoa.
Mkakati
wa pili ni kwamba atatumia uzoefu wake wa siku nyingi aliofanya kazi
serikalini kusaidia Chadema kupata wanachama katika uchaguzi wa serikali
za mitaa na uchaguzi mkuu 2015, kwani ana uhakika ana ushawishi mkubwa
kwenye jamii ya wtanzania.
Amesisitiza
kuwa “Chama ni wanachama, na chama ni vikao. Na Uimara wa Chama
chochote cha siasa unatokana na uimara wa Mabaraza yake ya Vijana,
wanawake na wazee. Ninao ushawishi wa kuifanya Chadema ikubalike na
kuungwa mkono na kupata wanachama nchini kote ndani ya Chama
nitashawishi mabaraza yapewe vitendea kazi ili yaimarike.
Ndani
ya chama nitaimarisha demokrasia, maoni na mtazamo tofauti ijadiliwe
hadi maafikiano yakubaliwe. Nitasimamia dhana ya Papa na Mkulima ni bora kuliko Papa peke yake.
Nitasimamia kauli mbiu ya Martin Luther King inayosema “Binadamu yeyote kama hajagundua jambo lolote ambalo hayuko tayari kufikwa nalo hafai kuishi.
Mimi
sitaki kuwa miongoni mwa wafu wanaotembea, nimeamua kuwapigania
watanzania masikini, wanyonge wanaonyanyaswa na utawala dhalimu wa CCM.
No comments:
Post a Comment