![]() |
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) EMMANUEL G. LUKULA |
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
Jeshi
la Polisi mkoani Dodoma limetoa tamko la kuzuia maandamano ya Chama cha
CHADEMA hapo tarehe 18/09/2014 na kuwataka wananchi kuyapuuza.
Akiongea
na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) alisema kuwa; Kufuatia
Viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya
Ofisi za Bunge Mkoani Dodoma kwa ajili ya kupinga Bunge la Katiba siku
ya tarehe 18/09/2014 linaloendelea, kuwa maandamano hayo ni batili na
akiwataka wananchi
wakazi wa Dodoma kuyapuuza kwa kuwa yanakiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.
wakazi wa Dodoma kuyapuuza kwa kuwa yanakiuka Sheria iliyoliweka Bunge hilo.
Kamanda LUKULA alitaja sababu za msingi za kuzuia maandamano hayo kuwa ni:-
1.
Siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi ikiwa ni pamoja
na muda wa maandamano hayo ni masaa ya kazi saa 04:00 asubuhi hadi saa
06:00 mchana yataathili ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
2.
Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo Kisheria na hakuna
tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha, hivyo moja ya
kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda Sheria na wale wanaofuata sheria.
Hivyo kufanya maandamano yanayopinga Bunge la Katiba ni kukiuka Sheria
iliyoliweka Bunge hilo.
3.
Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea, hadi sasa shauri
hilo linaendelea Mahakamani. Hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia
Uhuru wa Mahakama.
4. Baadhi ya Wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa Wakuu wa Polisi Wilaya kabla ya saa 24 kisheria.
Aidha
Kamanda Lukula alitoa wito kwa wananchi wa Dodoma kupuuza maandamano
yoyote ya kupinga uwepo wa Bunge la Katiba kwani ni batili. Aidha
aliwashauri viongozi wa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe
maandamano hayo na wasipo ridhika, wakate rufaa kwa Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi kwa maelekezo zaidi.
No comments:
Post a Comment