ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, September 19, 2014

Mhubiri aliyeteka roho za wengi Nigeria Huyu Hapa


Kanisa lililoporomoka mjini Lagos wiki jana , na kuwaua watu wengi, lilikuwa linamilikiwa na mhubiri anayesifika sana nchini Nigeria, TB Joshua.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anatufichulia haiba ya mhubiri huyu ambaye anadai amewaponya watu wakiwemo vipofu na waathiriwa wa HIV.
TB Joshua anadai kuwahi kutabiri matukio mengi kuanzia kwa kifo cha aliyekuwa gwiji wa muziki, Michael Jackson, hadi kupotea kwa ndege ya Malaysia ya MH370"
Anajiita mtume na ni mmoja wa wahubiri mashuhuri sana nchini Nigeria ambako makanisa kama lake ni mengi kupindukia.
Alizaliwa mwaka 1963 tarehe 12 Juni katika familia maskini, akidai kwamba alikaa kwenye tumbo la mamake kwa miezi 15.
Baadaye katika maisha yake, anadai kuona kwenye ndoto yake manabii wakimtaka kuhubiri na 


kufanya miujiza.
Hapo ndipo alipoanzisha kanisa lake analoiita, 'Church of All Nations (SCOAN),' mwanzoni likiwa na waumini 8.
'Maji ya kuponya'
Wanaume na wanawake waanguka sakafuni wakati wakiombewa na TP Joshua
Hii leo Jushua kama wahubiri wengine nchini Nigeria, ni tajiri wa kupindukia akishabikiwa sana na watu nchini humo.
Watu huja kwake kutoka kote duniani wakitaka kuombewa wapone.
Wakati ugonjwa wa Ebola uliporipotiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, serikali ya jimbo la Lagos, ilimtambua muhubiri huyo kwa kuambia wagonjwa wa Ebola kwenda kwake akawaponye.

Alikubali kuahirisha baadhi ya programu za kanisa lake za kuponya lakini inaarifiwa alituma chupa 4,000 za maji ya ''uponyo' nchini Sierra Leone anayosema kuwa yanatibu magonjwa mengi tu.chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...