ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Wednesday, September 3, 2014

POLISI WAMKAMATA AFISA USALAMA FEKI NA WAKAMATA BASTOLA NNE NA SHOTGUN MOJA


 Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.
 Kamanda Suleiman Kova akionyesha  silaha zilizokamatwa kwa wanahabari (hawapo pichani).

Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kova.
 JESHI la ×Polisi Kanda Maalum ya Dar es ×Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam,  kwa tuhuma za kujifanya  mtumishi wa ×Idara ya Usalama wa Taifa .
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara mwenye asili ya ×Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs 25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya ×Sheria ya Usalama wa Taifa.
Aidha jeshi hilo katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia silaha limefanikiwa kukamata  bastola nne na shot-gun moja wiki hii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...