ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Saturday, September 20, 2014

WALIOKUFA KWENYE KANISA LA NABII TB JOSHUA WAFIKIA 70

Idadi ya watu waliokufa kwenye ghorofa la makao makuu ya Kanisa la SCOAN (Synagogue Church of All Nations) la Nabii TB Joshua wamefikia 70.
Jengo hilo la ghorofa tano ambalo ni makao makuu ya kanisa na nyumba ya kulala wageni liliporomoka Jumamosi  wakati ujenzi ukiendelea.Afrika Kusini Pekee inahofia kuwa raia wake zaidi ya 60 wamefariki katika mkasa huu. Katika hali isiyokuwa ya kawaida, kumekuwa na mawasiliano hafifu kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo. Watu wameendelea kushangaa ni kwa nini Mtume Joshua hakuona hili likitokea wakati amekuwa akitegemewa sana na kuaminiwa kwa utabiri wake wa kuona vitu ambavyo vingetokea kabla havijatokea. Kwa mfano alitabiri kupotea kwa ndege ya Malasia na mambo mengine mengi. Serikali ya Nigeria pia inamtambua Nabii TB Joshua na hivi karibuni imewashauri watu wakatibiwe maradhi kama Ebola. Hata hivyo kutoka jamii ya kimataifa TB Joshua amekuwa akishutumiwa kwa kuwaaminisha wafuasi wake kuwa maji anayoyatoa yeye yanaponya magonjwa mbalimbali sugu hasa ukimwi.
A photo taken and released by Nigeria's National Emergency Management Agency (NEMA) on September 12, 2014 shows emergency workers transporting a man after he was pulled out from the rubble of The Synagogue Church of All Nations
Mmoja wa majeruhi waliookolewa kwenye kanisa hilo akiwa hajitambui.
Jengo hilo liko katika eneo la Ikotun magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lagos. 
 

LAGOS –

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...