Imetokea
nchini India baada ya mama mmoja kujifungua mtoto mwenye miguu minne na
mikono minne huku akipokelewa na wenyeji kwa furaha kubwa na kuitwa
‘Mungu Mvulana’
Mtoto huyo amepewa
jina la ‘Mungu Mvulana‘ kwa kuwa kuzaliwa na viungo kama hivyo si jambo
la kawaida na huchukuliwa kama mfano wa Mungu kwa jamii za kihindu na
watu walisafiri kutoka kona mbalimbali za nchi hiyo kwenda kumshuhudia
mtoto huyo wa maajabu.Katika mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo watu
walijazana nje ya eneo la Hospitali hiyo wakiwa na hamu ya
kutaka kumwona mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta baraka katika jamii zao.
kutaka kumwona mtoto ambaye ana maana kubwa kwa jamii za nchini humo na wenyeji wa huko wana amini ataleta baraka katika jamii zao.
Mamia ya watu walikua
wamejaza nje ya Hospitali hiyo wakiimba na kusali lakini hawakuweza
kufanikiwa kumwona kutokana na wingi wao huku Polisi wakitumia nguvu ya
ziada kuwazuia.
No comments:
Post a Comment