Gogo
akiwa darasani na wanafunzi wenziwe.Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke
wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita
inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi
duniani.
Akiwa
ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia
nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu
anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa
kiingereza kwenye daftari lake.
Prissilla
alijiunga na shule hii ya Leaders Vision Preparatory School miaka
mitano iliyopita lakini pia aliwahi kuwahudumia wakaazi wa kijiji chake
cha Ndalat kilichoko kwenye bonde la ufa kama mkunga miaka sitini na
mitano iliyopita.
Darasani
Priscilla anawasaidia wengine wafanye vyema ambao wana umri kati ya
miaka 10 hadi 14 na mar azote huwaambia ujumbe wake hasa mabinti kuwa
elimu ndiyo urithi wao.
Priscilla
anajulikana kama Gogo maana yake bibi katika lugha ya jamii ya
wakalenjini,anasefurahia masomo akiwa na umri wa miaka 90 katika umri
huo anajua kuandika na kusoma pia fursa aliyoikosa alipokuwa mdogo.
Lugha
ambayo Priscilla anajiona yuko huru kuitumia ni lugha mama kwake ki
Kalenjin kuliko kiingereza,pindi anapotakiwa kujieleza kwanini aliamua
kujiunga na shule katika umri wake.
Sababu
kubwa ambayo amekuwa akiitoa,ni ajue kusoma ili amudu kusoma
bibilia,lakini pia kwa umri wake anataka awahamasishe watoto kupata
elimu,kwani anawaona watoto wengi wakiwa hawako shuleni na watoto hao
wana watoto.
Gogo
apitapo mitaani haoni shida kukabiliana na watoto ambao hawako shuleni
katika muda wa masomo na kuwauliza kwanini hawako shuleni.
Gogo
anasema watoto hao humjibu kwamba hawaendi shule kwakuwa umri wao ni
mkubwa,name huwaambia mimi ni mkubwa sana kwenu lakini niko shuleni
hivyo nanyi jiungeni na shule.
Kikubwa
kinachomuumiza Gogo ni kuwaona watoto wengi waliopoteza muelekeo,wengi
wao hawana baba na wanazurura hovyo mitaani,bila msaada wowote.kutokana
na hali hiyo nataka kuwahamsisha waende shuleni.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment