Vita
dhidi ya Boko Haram vimeshika kasi tangu Chad ilipopeleka kikosi cha
wanajeshi wake kwenye mpaka wa Cameroon, katika mji wa Fotokol. Jumanne
mchana wiki hii, askari wa Chad wameingia katika mji wa Gamboru, nchini
Nigeria.
Wanajeshi
wa ardhini na magari ya kijeshi ya jeshi la Chad, ambayo yalikua katika
mji wa Fotokol, nchini Cameroon, wamevuka mpaka leo Jumanne mchana na
kupiga kambi upande wa pili wa daraja, katika mji wa Gamboru, nchini
Nigeria, uongozi wa jeshi la Chad umethibitisha leo Jumanne Februari 3.
Operesheni
hizo za ardhini zimefuatiwa na mashambulizi ya angani, ambayo yamedumu
takribani saa moja. Mji wa Gamboru, umeshuhudia mashambulizi ya majeshi
ya Chad na Cameroon kwa muda wa siku tatu mfululizo.
Boko
Haram ilikua iliuteka mji huo katika mashambulizi makali iliyoendesha
mwanzoni mwa mwezi Januari. Wakati huo wapiganaji wa Boko Haram
walishambulia ngome za wanajeshi wa Chad. Kwa kujibu mashambulizi hayo,
wanajeshi wa Chad walijaribu Jumamosi Januari 31, kuingia katika mji wa
Gamboru, kabla ya kuanza mashambulizi dhidi ya Boko Haram.
Jumatatu
wiki hii, viongozi wa Nigeria walithibitisha kwamba mji wa Gamboru uko
chini ya udhibiti wa majeshi ya Chad, jambo ambalo sio kweli, kufuatia
mapigano ya leo Jumanne asubuhi. Jumanne mchana, takribani wanajeshi
2000 wa Chad waliokua katika mji wa Fotokol, walionekana wakivuka mpaka
na kuingia Nigeria
No comments:
Post a Comment