ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, February 27, 2015

NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA

 

Ajali ya Ndege Mwanza
Ndege ya kivita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea jana Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda  alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu. 

Ajali ya Ndege Mwanza 
Ajali ya Ndege Mwanza
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa eneo la tukio kuangalia mabaki ya ndegevita hiyo iliyopata ajali leo.
Ajali ya Ndege Mwanza
Ajali ya Ndege Mwanza
Ajali ya Ndege Mwanza

 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...