ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, March 6, 2015

Waziri Magufuli aingizwa mkenge



Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli  



Siha. Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ameagiza kwa kusimamishwa kazi aliyekuwa kigogo wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) ambaye hafanyi kazi tena kituoni hapo.
Agizo hilo alilitoa juzi, huku akitaka pia mkurugenzi wa zamani wa majengo na miradi wa AICC, Paul Ndossa ambaye awali akifanya kazi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) akiwa mtaalamu na mshauri, asimamishwe.
Wakati Dk Magufuli akitoa agizo hilo, Ndossa alikuwa ameshaondoka AICC tangu Januari.
Agizo hilo lilitokana na Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakifugile kudai kuwa Ndossa ndiye aliyesimamia ujenzi wa majengo ya ofisi za wakuu wa wilaya za Siha na Moshi.
Majengo hayo mawili yanadaiwa kugharimu mabilioni ya shilingi, lakini yalijengwa chini ya kiwango tangu yalipokamilika miaka mitano iliyopita na hayafai kwa matumizi ya kiofisi.
Hata hivyo, Ndossa alipotafutwa kuzungumzia madai hayo alishangazwa na kutuhumiwa kuwa alikuwa mtaalamu mshauri wa miradi hiyo.
Ndossa alisema waziri atakuwa amepewa taarifa potofu.
“Mimi sikuwa consultant (mtaalamu mshauri) wa ujenzi wa hilo jengo (la Siha). Consultant wa mradi walikuwa TBA, Makao Makuu...waliitumia ofisi ya Kilimanjaro mimi sikuwa Moshi.
“Nilikuwa nakwenda kule kusaidia tu. Wakati wa kufanya Site meeting (vikao eneo la mradi). Mimi nilikuwa Arusha nitakuwaje consultant Kilimanjaro? Watakuwa wamempotosha Waziri,” alisisitiza Ndossa.
Licha ya kukana, wakati Dk Magufuli akikagua jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya Siha, alielezwa kuwa, ujenzi wa jengo hilo uliokuwa chini ya viwango na ulisimamiwa na Ndossa .
Mwakifugile alisema malighafi zilizochanganywa katika ujenzi huo, zilipunguzwa tofauti na viwango vilivyotakiwa.
“Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na vyombo husika, hii slab ilitakiwa ijengwe milimita 175, badala yake imejengwa milimita 150, lakini pia hata malighafi haikuwa imefikia kiwango kinachotakiwa,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...