ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AU WAFUNGULIWA JANA ADDIS ABABA. Show all posts
Showing posts with label MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AU WAFUNGULIWA JANA ADDIS ABABA. Show all posts

Thursday, January 30, 2014

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AU WAFUNGULIWA JANA ADDIS ABABA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye Mkutano wa  Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) ambao  umefunguliwa  rasmi  leo tarehe 30 Januari, 2014 mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mwenyekiti wa Kamisheni  ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma akisoma hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja huo mjini Addis Ababa, tarehe 30 Januari, 2014. Katika hotuba yake Dkt. Dlamini-Zuma alisisitiza umuhimu wa matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwani ni moja ya lugha kubwa Barani Afrika.na matukioissamichuzi
Jopo la Marais Wastaafu wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mhe. Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Nigeria, Mhe. Thabo Mbeki, Rais  Mstaafu wa Afrika Kusini na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana.
Rais Mpya wa Madagascar, Mhe. Henry Rajaonarimampianina akitoa hotuba yake ya shukrani kwa nchi za Afrika kwa michango yao iliyopelekea uchaguzi wa amani na demokrasia nchini Madagascar na pia kwa  Madagascar kurejea AU.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. hailemariam Dessalegn akitoa hotuba kama Mwenyekiti wa AU  anayemaliza muda wake kabla ya kukabidhi nafasi hiyo kwa Rais wa Mauritania, Mhe. Mohamed Ould Abdel Aziz.
Rais wa Mauritania, Mhe. Mohamed Ould Abdel Aziz  akitoa hotuba kama Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi Januari 2015.
Picha ya Pamoja ya Viongozi wa AU.
Mhe. Membe akiongozana na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa AU
Mhe. Membe akiteta jambo na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma nje ya Ukumbi wa Mikutano wa AU. 

Kiswahili chazidi kupaa Umoja wa Afrika

Na Mwandishi wetu, Addis Ababa

Umoja wa Afrika umeitaja Lugha ya Kiswahili kuwa ndiyo lugha kubwa na rasmi Afrika na ndio Lugha inayofundishwa zaidi katika Vyuo Vikuu mbalimbali duniani kutoka Afrika.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...