Waislamu nchini Tanzania Leo Julai 10 wanaungana na waislamu kote duniani kuanza Mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mufti wa Tanzania Shaban Issa Bin Simba imesema kuanza kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kunafuatia kuandamwa kwa mwezi ikiwa ni kiashirio tosha kuanza kwa ngwe hiyo.
Hata hivyo Mufti Shaban Issa Bin Simba amewataka Waislamu wote nchini kujikita kumpenda Mungu siku zote za Mfungo na hata baada ya mfungo.
Goldentz inawatakia Waislamu wote Mfungo mwema na wenye Baraka.