ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI
Showing posts with label william ruto. Show all posts
Showing posts with label william ruto. Show all posts

Wednesday, October 23, 2013

Kenya yasubiri jibu la Umoja wa Mataifa

kenya 988f0
Kenya imewasilisha rasmi barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuahirisha kesi zinazoendelea katika mahakama ya ICC dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto. Pia, nchi 49 za Umoja wa Afrika zimetia saini barua iliyowasilishwa Jumanne kwa baraza hilo ikiunga mkono kuahirishwa kwa kesi hizo dhidi ya viongozi wa Kenya. (HM)

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Jumatano, balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa bw. Macharia Kamau alisema Kenya na Umoja wa Afrika wanasubiri kwa hamu maamuzi ya baraza hilo.
Katika ombi lake Kenya inalitaka baraza hilo kufikia maamuzi ya haraka kuwawezesha viongozi wake kutohudhuria vikao vya kesi dhidi yao katika mahakama ya The Hague kwa mwaka mmoja.
Balozi Kamau alisema Kenya inakabiliwa na tishio kuu la ugaidi na ukosefu wa usalama hata kutoka pembe ya Afrika. Alisema ombi la Kenya la mwaka wa 2011 katika baraza hilo halikupata majibu yaliyotegemewa na kwamba viongozi wake bw. Kenyatta na naibu rais Ruto wanahitaji kuwa nchini kusimamia shughuli za usalama na majukumu yao kama wanavyotakiwa na katiba ya nchi hiyo.
Viongozi hao wa Kenya wanakabiliwa na mashtaka mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC kwa tuhuma kwamba walichochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 na mapema mwaka wa 2008.
Kesi dhidi ya naibu rais Ruto imekuwa ikiendelea, huku kesi dhidi ya bw. Kenyatta ikitazamiwa kuanza Novemba 12 mwaka huu. Aidha balozi Kamau anasema anatazamia maamuzi ya baraza hilo yatafikiwa kwa wakati ili rais huyo aweze kupanga mikakati ya ulinzi wa taifa lake ambao ni muhimu sawa na wa nchi nyingine zote za dunia. Chanzo: voaswahili

Tuesday, September 17, 2013

Shahidi wa kwanza atoa ushahidi ICC

zzzzzzzzzWilliam_Ruto_in_th_2665831b_3eda6.jpg
Shahidi wa kwanza kutoka upande wa mashtaka, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC kutoa ushahidi dhidi ya naibu Rais wa Kenya William Ruto.
Mahakama inamlinda shahidi huyo kwa kutoonyosha sura yake.
Ruto anakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008(P.T)
Kesi dhidi ya Ruto na mshtakiwa mwenzakeJoshua Arap Sang, ilianza tarehe 10 mwezi Septemba, baada ya wawili hao kutuhumiwa katika kuhusika na ghasia hizo za mwaka 2007.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mashahidi kujiondoa kwenye kesi hiyo wakihofia usalama wao. Mwishoni mwa wiki, mashahidi wanne walijiondoa katika kesi hiyo baada ya kuelezea wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwa watatoa ushahidi mbele ya mahakama hiyo.
Wiki jana mkuu kwenye kesi hiyo, aliakhirisha kesi hiyo kwa sababu mashahidi hawakuwa wamefika kwenye mahakama hiyo kutoa ushahidi wao.
Rais Uhuru Kenyatta, anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novmba kwa mashtaka sawa na hayo.

Tuesday, July 16, 2013

Ombi la makamu rais wa Kenya lakataliwa ICC.

Rais wa Kemya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Rutto walipokwenda mahakamani ICC Aprili 2011.
Rais wa Kemya Uhuru Kenyatta na makamu wake William Rutto walipokwenda mahakamani ICC Aprili 2011.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imekataa ombi la makamu rais wa Kenya kutaka kesi yake ianze kusikilizwa Afrika. ICC imesemajana Jumatatu kuwa kesi ya makamu rais wa Kenya William Rutto itaanza kusikilizwa mwezi Septemba huko Hague katika makao makuu ya  ICC.

Ruto na mshitakiwa mwenzake Joshua Arap Sang wanashitakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kwa kusaidia kufanya ghasia mbaya za kikabila zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Mawakili wa utetezi waliiomba ICC kusikiliza walau sehemu ya kesi hiyo nchini Kenya au Tanzania.   Taarifa ya ICC inasema majaji walikubali  kimsingi  wazo hilo lakini wameamua kusikiliza kesi hiyo Hague kwa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na usalama, gharama na athari kwa mashahidi na waathirika.

Uamuzi huu wa jana hautaathiri kesi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye anakabiliana na mashitaka ya uhalifu  dhidi ya ubinadamu kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi  nchini Kenya.  Kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Novemba 12.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...