Akibariki waumini
Ibada ya Kumsimika Papa Tawadross II iliyofanyika leo
Papa akitoa mahubiri
Papa akimega mkate
Akiwa na maaskofu wenzake kabla ya kutangazwa kuwa papa
Wakristo wa Misri wakimshangilia Papa wao Mpya
Rais Morsis wa Misri akiongea na Papa
Papa mtakatifu mpya wa Kanisa la Coptic nchini Misri ametawazwa rasmi hii leo mjini Cairo.
Papa Tawadros II, alithibitishwa rasmi kuwa
kiongozi mpya wa Wakristu waliowachache, katika sherehe iliyofanyika
katika kanisa la St. Mark, mjini Cairo.
Kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 60, anachukua mahala pa Papa Mtakatifu
Shenouda III, ambaye aliaga dunia mwezi Machi mwaka huu, baada ya
kuliongoza kanisa hilo kwa miongo minne iliyopita.
Kutawazwa kwake kumejiri wakati wakristu nchini
humo wakiwa na wasi wasi mwingi kufuatia kuondolewa madarakani kwa rais
Hosni Mubarak mwaka uliopita.
Taifa hilo limeshuhudia mashambulio kadhaa dhidi
ya waumini wa kanisa hilo na pia makanisa kadhaa nchini humo
yameshambuliwa tangu kuporomoka kwa utawala wa rais Mubarak.
Raia wengi wana shaka nyingi kuhusiana na kuibuka kwa makundi mengi ya Kiislamu.
Inakadiriwa kuwa Wakristu nchini Misri ni kati
ya asilimia 5-10 ya idadi yote nchini humo ambao wengi ni waislamu wa
dhehebu la Kusini.
Misri ndilo taifa la pekee katika eneo la Mashariki ya Kati iliyo na idadi kubwa zaidi ya wakristu.
Rais wa nchi hiyo ambaye ni muumini wa dini ya
Kiislamu Mohammed Mursi hakuhudhruia sherehe hiyo lakini waziri wake
mkuu Hisham Qandil alikuwepo.
No comments:
Post a Comment