ndege za kivita za Israel
Ndege ya Kivita ya Israel ikiachia kombora kulenga maeneo ya Gaza
na wafanyakazi wa afya
Kikosi cha Zimamoto cha Gaza kikijaribu kuzima moto katika mabaki ya nyumba zilizobomolewa na makombora ya Israel
Makombora ya Israel yakishambulia maeneo mbalimbali ya Gaza
Majeruhi akikimbizwa hospitalini
Mabaki ya nyumba za Wapalestina
Hili ni Kombora lililorushwa na wanamgambo wa Hamas likielekea Israel ambapo pia hadi sasa watu watatu wameuwawa
Kombora la Israel lipelipua Makao makuu ya Hamas
Askari wa Israel wakiwa katika Doria
Uharibifu wa makombora ya Israel
Wapalestina wakiwazika wafu wao
Kiongozi wa wanamgamo wa Hamas auwawa katika shambulio la anga la Israel lililolenga gari lake
Akina mama na watoto wanakufa
Watoto wasiokuwa na hatia nao wauwawa Gaza
Shambulio la kombora kiliacha uharibifu mkubwa
Mwanamke wa Palestina akiomba dua baada ya makazi yake kusambaratishwa na maoketi ya Israel
Katika siku ya sita mfululizo, makombora ya Israel yanaendelea kumiminika katika Ukanda wa Gaza ambapo uharibifu mkubwa umetokea pamoja na kupeteza maisha ya wanamgambo wengi wa kundi la hamas wameuwawa. Leo ameuwawa kiongozi mkuu wa kijeshe wa wanamgambo hao aitwaye Ramez Harb. Hadi kufikia leo, Wapalestina 94 wameshauwawa na mashambulio ya ndege za Israel. Kwa upande wake, Israel inasema itafanya kila iwezacho kuhakikisha inalinda usalama wa raia wake ambao wako hatarini kuuwawa na makombora ya Hamas ambapo hadi sasa yameshauwa Waisrael watatu. Duru za Kijeshi za Israel zinasema kuwa Jeshi limeweza kuzuia zaidi ya makombora 40 yaliyorushwa na Wapalestina kuelekea katika makazi ya watu. Nchi za Uturiki na Quater zinajaribu kutafuta usuluhishi wa kidiplomasia ili kuzuia ghasia zaidi zisiendelee kusambaa hasa wakati huu ambapo jirani zao Syria nayo ipo katika hali mbaya sana ya machafuko ya vita vilivyodumu kwa takriban miezi 19 na kugharimu uhai wa watu zaidi ya 36,000.
Hata hivyo kundi la wanamgambo wa hamas wanaendelea kutamba kuwa Israel ndiyo kwanza imejifungulia lango la kuzimu. Soko la mafuta limeendelea kupanda kutokana na mgogoro huo unaoendelea kushika kasi Mashariki ya Kati
No comments:
Post a Comment