Mtoto akiwa chini ya handaki kujilinda na makombora
Mapigano yameendelea usiku kucha katika eneo la Gaza licha ya fununu kuwa kumewekwa mkataba wa kusitisha mashambulio.
Israel inadaiwa kuendeleza mashambulio hayo katika maeneo kadhaa ya Gaza yaliyosababisha kupoteza kwa nguvu za umeme.Takriban wapalestina ishirini wameripotiwa kuuawa .
Hapo jana Israel ilisambaza ilani kuwaonya wakaazi waliokuwa pembezoni mwa Gaza, wahamia katikati mwa jiji kwa usalama wao.
Isarel imesema kuwa wapiganaji wa kipalestina wamerusha zaidi ya makombora mia na hamsini kwenye ardhi yake tangia Jumanne.
No comments:
Post a Comment