Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, amesema yuko tayari kuchunguza malalamishi ya wapiganaji wa
waasi ambao wameuteka mji wa Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Akiongea baada ya mazungumzo yaliyofanyika
nchini Uganda na Kuhudhuriwa na rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Joseph
Kabila amesema anatathmini uwezekano wa kuanzisha mazungumzo na waasi
hao wa M23.
Mwenyekiti
na mwenyeji wa Mazungumzo hayo, rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais
Kabila na Kagame kwa kauili moja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano
hayo na pia kutoa amri kwa waasi hao kuondoka Goma mara moja.
Awali wapiganji hao wa waasi walitishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.
Hapo jana, wapiganaji hao wa M23 waliuteka mji wa Sake, ulioko takriban kilomita 27, kutoka Goma.
Ripoti zinasema wapiganaji hao sasa wanajiandaa kuelekea eneo la Kusini hadi Bukavu, takriban kilomita 230 kutoka Goma.
Ripoti zinasema wapiganaji hao sasa wanajiandaa kuelekea eneo la Kusini hadi Bukavu, takriban kilomita 230 kutoka Goma.
Kamanda mmoja wa waasi hao, aliliambia umati wa
watu waliokusanyika katika uwanja wa michezo mjini Goma, kuwa safari yao
ya kukomba taifa hilo imeanza.
Kundi hilo la M23 liliundwa mwezi April mwaka huu baada ya wanajeshi kadhaa kuasi.
Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009.
Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009.
Vitendo vya wapiganaji hao wa M23, vimezua wasi
wasi wa kuzuka upya kwa mapigano nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, ambako takriban watu milioni tano waliauawa kufuatia mapigano
yaliyoanza mwaka wa 1997 na kumalizika mwaka wa 2003.
No comments:
Post a Comment