Wananchi wa kijiji cha
Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa
kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko
ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.
Mkazi wa Kata ya Mliiba,
Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bi. Grace Nyakola (33) akisoma nakala ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi
wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo, leo
alhamisi Nov. 22, 2012.
Mjumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa
vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime
mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22,
2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda
na Riziki Ngwali.
Wananchi
wa Kata ya Mliiba Wilayani Tarime mkoani Mara wakisoma nakala za Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na machapisho mbalimbali
yanayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na
Tume hiyo katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22, 2012
Na Ismail Ngayonga, Tarime, Mara
MKAZI wa Kata ya Kata ya Mliiba
Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marco Magubo (31) amependekeza ni vyema Katiba
Mpya ikataze vyama vya siasa vinavyoingia madarakani mara baada ya kushinda uchaguzi
wa Rais visipeperushe bendera yake na badala yake kuweka bendera ya Taifa.
Akitoa maoni yake leo (Alhamisi Nov. 22, 2012) kuhusu Katiba
Mpya kwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alisema kitendo cha
kupeperusha bendera ya chama kilichoingia madarakani kitaongeza chuki kwa
wanachama wa Chama kingine cha siasa kilichoshindwa uchaguzi.
Aidha Magubo alisema Rais
anayeingia madarakani anawakilisha maslahi ya wananchi wote na hivyo si busara
kwa Chama kilichoshida uchaguzi kupeperusha bendera ya Chama chao kwani Kiongozi
huyo haongozi wanachama wa chama chake pekee bali wananchi wote katika taifa.
“Tazama Marekani ambao hivi
majuzi tu walifanya uchaguzi mkuu wa Rais, katika kampeni za vyama vyao
hatukuweza kuona bendera ya Republican wala Democracy ambavyo vyote vilishiriki
uchaguzi na badala yake tuliona wananchi wakipeperusha bendera ya Taifa lao na
hatukuona bendera ya Republican wala Democracy” alisema
Alisema kwa kuwa Tanzania ni nchi
ya umoja, amani na mshikamano ni vyema
Katiba Mpya ikewe kipengele cha kukataza bendera za vyama vyao na badala
ya wamwachie Kiongozi aliyopo madarakani kutetea hoja za wananchi wote.
No comments:
Post a Comment