Meneja wa Swahili Fashion Week, Washington Benbella akizungumza na waandishi
wa Habari wakati wa uzinduzi wa Swahili Fashion Week 2012. Kutoka kushoto ni
Happy Shame Meneja Masoko EATV na Catherine Ndabanga Afisa Masoko na Mauzo
Golden
Onyesho kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati
linarajiwa kufanyika siku tatu mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia
tarehe 6, 7 na 8 Desemba, 2012 ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja
wadau 50 katika tasnia ya Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na
nyengine kuweza kuonyesha ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia
ya mitindo katika ukanda huu.
“Mwaka tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka
Tanzania wataweza kuonyesha ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya
Tanzania, ambao wote wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia
wabunifu 16 walionyesha ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion Week
yaliyofanyika Nairobi, Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa Swahili Fashion
Week, Washington Benbella
Katika kuongeza maonyesho ya mitindo, mwaka huu Swahili
Fashion Week shopping Festival ambayo ilianza 2010 itakuwepo tena kwa mara
nyengine ambapo itashirikisha zaidi ya waonyeshaji 30 katika sehemu moja ikiwa
ni kwa ajili ya kuonyesha na kuuza bidhaa za ubunifu hivyo kuifanya kuwa msimu
mkubwa manunuzi ya kazi za ubunifu wa mitindo hapa Tanzania.
Kama ilivyo ada, Swahili Fashion Week inatoa nafasi kwa
kuendeleza vipaji, ambapo tarehe 24 Novemba, 2012 kutakuwa na mchujo wa wazi kwa
wanamitindo wapya na wanaochipukia kwa jinsia zote, na mnamo tarehe 7 Desemba,
2012 kutakuwa na warsha kwa ajili ya wabunifu wote Tanzania chini wadhamini
wakuu wa warsha hiyo USAID Compete ambayo itafanyika katika Hotel ya Golden
Tulip” Aliongeza Benbella
Mashindano tofauti yamepangwa kufanyika wakati wa Swahili
Fashion Week, ikiwemo Shindano la kumtafuta Mbunifu Bora anaechipukia na Mbunifu
Bora wa kubuni Fulana. Sio tu inatoa changamoto na ari ya ushindani katika
tasnia ya ubunifu nchini Tanzania, bali pia inaweka msingi imara kwa wabunifu wa
baadae.
“Sherehe maalum za kufungua Swahili Fashion Week
zinarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Novemba, 2012, Thai Village
kuanzia saa 9 usiku. Sherehe hizo pia zitafuatiwa na kutangazwa kwa majina ya
waliochaguliwa kushindania tuzo mbalimbali zilizowekwa katika vipengele 16, tuzo
hizi ni za kwanza na ndio pekee katika ukanda huu. Tiketi za sherehe za uzinduzi
wa Swahili Fashion Week 2012 zinapatikana sehemu zifuatazo, Thai Vilage, Mgahawa
wa Epidor uliopo Masaki, na Tanzania Mitindo House” Alisema Meneja Uhusiano,
Hassan Mrope
“Tukiwa na mipango yenye ndoto za kutangaza biashara ya
mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, ninapenda kuchukua nafasi hii
kuwashukuru washirika wetu pamoja na wadhamini wetu ambao karibia
ya wote wamekuwa wakitusaidia kutokea maonyesha yaliyopita mpaka sasa.
Pia
tuwashukuru sana watu wote wanaosaidia tasnia ya mitindo hapa Tanzania kwa si tu
kuhudhuria matamasha na maonyesho kama haya bali pia kwa kununua bidhaa
zinazotengenezwa hapa nchini kwani hii inatangaza kinachotengenezwa Africa “Made
in Africa”. Alimalizia Benbella
Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na Vodacom, USAID
Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula,
Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites,
Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania),
Perfect Machinery Ltd, Ndibstyles, PKF Tanzania and 361
Degrees.
No comments:
Post a Comment