Mjumbe
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Mwantumu Malale (kushoto) akisalimiana na
Katibu Tarafa wa Kata ya Mbulumbulu Wilayani Karatu mkoani Arusha, Tatu Eliasi jana
jumatatu Novemba 19, 2012 wakati wajumbe wa Tume hiyo walipofika katika Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji maoni ya
wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani humo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya
Karatu, Daudi Ntibenda
Mkazi
wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani
Arusha, Thimos Mushi (51) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa
mkutano wa kukusanya maoni ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
kijiji hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi
kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha
Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya
Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni
ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19,
2012.
Akina Mama wa kijiji cha
Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya
wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo jana
jumatatu Novemba 19, 2012.
Wananchi wa Kata ya Rhotia
Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni kuhusu
Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo jana
jumatatu Novemba 19, 2012.
Tembelea
No comments:
Post a Comment