ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Monday, January 14, 2013

BALAA LINGINE IFM, WAPATA MKONG'OTO KUTOKA KWA JESHI LA POLISI, Ni baada ya kukaidi kuondoka kwenye kituo cha Polisi Kigamboni


 

Askari Polisi ambaye hakuwa kwenye sale za jeshi hilo akimsulubu mmoja wa wanafunzi wa IFM baada ya kudhibitiwa kwenye eneo la kituo cha Polisi Kigamboni walipofika kutaka kulazimisha kufanyika mkutano wao na kamanda Kova badala ya eneo lililopangwa kwenye viwanja vya Machava. Wanafunzi hao walikamatwa baada ya kupigwa mabomu ya machozi kwenye eneo hilo na kukamatwa kama kuku wa mdondo.
Askari wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi.
Kundi la wanafunzi walishikwa kama kuku wa mdondo baada ya kupigwa mabomu ya machozi na kujikuta wakijificha sehemu moja kundi zima hali iliyosabisha kutembezwa kichurachura hadi kwenye kituo cha Polisi cha Kigamboni.
Mwanafunzi huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi.
Mwanafunzi huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni.
Kichapo kilipozidi hakukua na mtu aliyejali kama notes zake zinapotea kila mmoja alitarazaq juu ya maisha yake.
Baada ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako waalijificha wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi ili wajisalimishe.
Huyu alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga.
Hapa amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini.
Huyu hakujiweza kabisa mabomu yalimchanganya na kudondoka toka kwenye Difenda ya Polisi.
Virungu vilitumika kushindilia watu kwenye Difenda.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...