Sentahafu
wa Zambia Stopilla Sunzu amechukua likizo fupi kutoka kwenye kambi ya
timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2013 ili apate nafasi ya
kwenda nchini England kwenda kufanya vipimo vya afya kwa ajili ya
kujiunga na klabu hiyo.
Sunzu
ambaye anachezea klabu ya TP Mazembe ya DRC ambayo imeandika kwenye
mtandao wake kwamba ada ya uhamisho ya $4.8million imeshakubaliwa na
kilichobakia ni mchezaji kukamilisha vipimo vya afya.
Mfungaji huyo wa penati ya
ushindi ya Zambia dhidi ya Ivory Coast katika AFCON 2012, anatarajia
kurudi Afrika ya kusini January 19, siku mbili kabla ya mabingwa
watetezi kuchuana na Ethiopia katika mechi ya ufunguzi.
No comments:
Post a Comment