Wanajeshi watiifu kwa Asaaad wakipambana na waasi eneo la Aleppo's al-Liramun
Waasi wa Halab al-Shabah wakiwalenga wanajeshi wa Assad neneo la Al-Amariya Aleppo
Wanajeshi wa Rais Assad wakikatiza kwa stail eneo ambamo wapo waasi walenga shabaha walijificha katika majengo eneo la Tal al-Zarazi Aleppo
Mmoja wa waasi wanaompinga Asaad akiwa ameshikilia silaha ya kirusi waliyoiteka kwa wanajeshi wa SerikaliAkaskazini Masharika mwa mji wa
Maraat al-Numan
Ndege aina ya Sukhoi-22 inayomilikiwa na Serikali ikidondosha bomu lenye uzito wa fi500lb katika mji wa Maraat al-Numan
Mwanaume amekaa kwa kuchoka baada ya kuangalia iliyokuwa nyumba yake na workshorp ikiwa imeharibiwa kabisa na bomu kutoka katika ndege eneo la Maaret al-Numan in southern Idlib
Mnzee akiangalia samani za ndani zilizobaki baada ya ndege za Asaad kupitia nyumba yake katika eneo la Maraat al-Numan
Waazi wakikanyaga kwa kulaani picha za Rais Assad katika mitaa ya Alepo ya Zamani
Baadaye wametumia picha hizo kupikia chai
Wananchi wakifurahia na kuchezea kifaru kilicholetwa na wanajeshi wa Assad ambao waliasi na kujiunga na upinzani katika eneo la Atareb karibu Aleppo
Waasi na wapita njia wakiangalia Buldoza kilifanya usafi eneo la Hospitali ya Dar Al-Shifa huko Aleppo
Timu ya uokoaji iliangalia kama kuna wagonjwa walionusurika baada ya ndege za Assad kulipua hospitali ya Dar Al Shifa huko Aleppo
Mtoto akisaidia kufanya usafi katika hospitali ya Dar Al-Shifabaada ya kupigwa bomu
Wakati huo huo, askari wa wardhini wa Assad wanajiandaa kupeleka mashambulizi zaidi baada ya ndege kulipua maeneo mengi katika maeneo ya Alepo ambayo yanadhibitiwa kwa kiasi kikubwa na waasi
Mwanajeshi wa upande wa waasi akiandaa bomu la kutengeneza kwa mkono kabla ya kulilipua kwa wanajeshi waasi
Raia wakiwa hawaamini uharibifu wanaouona uliotokana na mashambulizi ya ndege za Srikali huko Khaldiyeh katika mkoa wa Homs
Huu ni uharibifu wa makombora ya ndege katika maeneo ya karibu na Damascus
Waasi wakiwa katika vyumba vya chini ya ardhi katika makumbusho ya al-Maraa ambayo ni makumbusho makubwa zaidi duniani ya kipindi cha utawala wa Kirumi katika mji wa Marat
al-Numan, Aleppo
Makombora yalilenga Chuo kikuu cha Alepo ambapo wanafunzi 80 waliuwawa wakiwa kwenye mitihani
Huyu ndiye Rais Baashar Al- Asaad ambaye familia yake imetawala kwa miaka zaidi ya 40 kwa mabavu na ambaye wananchi wengi wa Syria wameanza kumpinga tangu miaka miwili iliyopita. Inakadiriwa zaidi ya watu 60,000 wameshakufa na kadiri siku zinavyosonga mbele na kadiri waasi wanavyozidi kumsogelea Assadr damascus ndivyo nanavyozidi kuwaangamiza bila huruma. Inasemekana kwamba yale mabomu ya kibaiologia ambayo syria inayo ameshayaweka tayari kwa kuyatumia na hiyo ndoyo silaha yake ya mwisho. Kwa sasa uwezekano wa kuwashinda waasi ni mdogo sana kwani asilimia 80 ya raia wote hawamtaki na wanaungwa mkono na nchi za magharibi pamoja na nchi nyingi za uarabuni. Kwa upande wake, Asaad ambaye anatoka katika kabila dogo lenye nguvu la Alawite, anaungwa mkono na Iran, Hesbolah, Urusi na China. Kuingia kwa Urusi katika mzozo huo kumewafanya wamabe wa Magharibi yaani Marekani na washirika wake kuogopa kuingilia moja kwa moja kama walivyofanya kwa Ghadafi. Hata hivyo Uruhi na uchina wameshaanza kuwaondoa wafanyakazi wao huko Syria kwani nafasi ya Rais Assad kuishinda nguvu ya Umma ambayo imeshaamua kwamba ziwe mbivu ziwe mbichi ni lazima aondoke. Inakadiriwa ndani ya mwezi mmoja ujao Asadi anatakuwa hana tena akiba katika benk kuu hivyo au apewe misaada na Iran na Urusi au atoroke. Hata hivyo nafasi ya yeye kutoroka ni ngumu kwani waasi wameshazunguka viunga vyote vya mji mkuu na wanajeshi waliopo mikoani nao wamezungukwa hivyo hali kuendelea kuwa ngumu kwa Bwana Asaad. Marekani hata hivyo ilimwonya Asaad kwamba kama atajaribu kutumia silaha za kemikali alizo nazo basi ndipo atakapojua Obama ni nani.
No comments:
Post a Comment