Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid
(mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa
kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea
Arusha kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan.
17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje
ya nchi. (picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama
Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya
ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini
Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya
Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo
anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. (Picha na Mwanakombo Jumaa-
MAELEZO).
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya ngoma mbalimbali
za utamaduni alipowasili katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha
Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya
Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Aliengozana nae
wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora
Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Kikundi
cha kinamama cha ngoma ya Msanja kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
salma Kikwete (hayupo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa
Kilimanjaro (KIA ) Jan 16,2013.(Picha na Mwanakombo Jumaa wa
MAELEZO).
Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma
Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)
wakati alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA)
Jan 16,2013.- Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama
Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John
Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan
16,2013. –Picha na Mwnakombo Jumaa- MAELEZO.
………………………………….
Mahmoud Ahmad Arusha
Kauli mbiu ya kongamano la ulimwengu la Afya ya uzazi
linaloendelea jijini Arusha imepewa msisitizo na kuwa hakuna mama
atakayekufa wakati akileta kiumbe duniani na pia Afya ya mama na mtoto
ipewe kipaumbele.
Kauli hiyo imeendelea kutolewa na Mke wa Rais mama Salma
Kikwete wakati akiwasilisha na kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo
jijini hapa na kuwataka watafiti na wataalamu hao kuja na majibu
yatakayosaidia kupunguza vifo vya wakinamama wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment