Rais
wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki amesema mtangulizi wake Mzee
Nelson Mandela, huenda akatoka hospitali na kuendelea na matibabu
nyumbani.
Mbeki amesema hayo wakati akizungumza katika hafla moja ya Chama cha Afriacan National Congress-ANC.
Mandela
amelazwa hospitali kwa wiki tano sasa kutokana na maambukizi ya
mapafu, hali iliosababisha kumiminika kwa risala za kumuombea nafuu
kutoka ndani ya Afrika Kusini na kimataifa.
Marafiki waliomtembelea wamesema Mandela bado anapumua kwa msaada wa mashine.
Shujaa
huyo wa vita dhidi ya sera ya ubaguzi wa rangi, alitumikia kifungo cha
miaka 27 gerezani, kabla ya kuwa Rais wa kwanza wa Afrika kusini ya
Kidemokrasia mwaka 1994.
Thabo
Mbeki aliyekuwa makamu wake wa Rais, alishika wadhifa huo wa kuiongoza
Afrika kusini wakati Mandela alipostaafu mwaka 1999.
Ifikapo siku ya Alhamisi wiki hii Mandela atatimia umri wa miaka 95.
No comments:
Post a Comment