Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi
upokeaji wa mabomba ya gesi tayari kwa kusafirishwa hadi Mtwara.
Waziri
Mkuu Mh. Mizengo Pinda akibadishana mawazo na Waziri wa Nishati na
Madini Prosefa Sospeter Muhongo aliyekaa kushoto. Kulia ni Balozi wa
China nchini Tanzania Lu Youging wakati wa hafla ya kuzindua kupokea
shehena ya mabomba kwa ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam.
Mh.
Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu
Youging alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara ya uzinduzi
rasmi wa upakeaji wa mabomba ya Gesi.
Pichani ni mafundi wakiwa katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari kwa safari ya Mtwara.
Balozi
wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging akifafanua jambo. Kushoto
ni Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo.
Na Frank Shija – Maelezo
Serikali imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba
ya gesi kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara
hadi Dar es Salaam.
Pinda
amesema kuwa wananchi wa Tanzania watanufainaka na mradi huo hasa
wakazi wa Mtwara kwa kuwa vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya
kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwa kuwa viwanda mbalimbali
vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake
umekwisha anza.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchiniTanzania Lu
Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huo, na kukua kiuchumi
kwa kuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala
yake itazalisha nishati yakutosha.
Balozi
huyo ameongeza kuwa kupitia mradi huo Tanzania itaondokana na kuwa
tegemezi katika shughuli zake za maendeleo, kwa kuwa kuna hazina ya
kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si
vinginevyo.
Jumla
ya mabomba 3,400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya
pili itapokelewa shehena yenye mabonmba 4,600 katika bandari ya Mtwara.
Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi utakapokuwa umekamilika.
No comments:
Post a Comment