Jose
Mourinho ametoa ishara kwamba klabu yake ya Chelsea inaweza kutuma ofa
ya kumsajili mshambuliaji wa kikolombia Radamel Falcao mara tu dirisha
la usajili litakapofunguliwa.
Meneja huyo wa Chelsea hakuonyesha kuficha matamanio yake ya kumleta
mshambuliaji huyo wa Colombia darajani – Falcao ambaye kwa sasa ni
majeruhi wa goti – ameripotiwa kwamba anataka kuondoka kwenye ligi kuu
ya Ufaransa kutokana na kutokuwepo kwa ushindani kwenye ligi hiyo.
Katika mahojiano na Canal Football Club, Mourinho aliondoa uwezekano
wa klabu yake kuwasajili washambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic na
Edinson Cavani, akisisitiza ni ‘haiwezakani’ kuwasajili wachezaji hao.
Alisema: ‘Nina timu, lakini sina mshambuliaji. Falcao hana timu pale.
Mchezaji kama yeye hawezi kuwa anacheza mbele ya mashabiki 3,000.
Monaco ni klabu ya kumalizia soka, hampafai pale kwa sasa.”
Falcao, 28, alijiunga na Monaco kwa ada ya £50million kutoka Atletico Madrid kipindi cha kiangazi kilichopita.
No comments:
Post a Comment