Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
Dar es Salaam, Tanzania
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ametangaza kuwang’oa viongogo
wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na
kutoridhishwa na utendaji wao.
Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu, kama alivyolisoma jana na theNkoromo Blog kupata nakala ya tamko hilo
Leo,
TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya
Wanyamapori ya Wizara ya maliasili na Utalii kama ifuatavyo:
Ninamuondoa
Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya
Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Nachukua hatua hii
kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo
katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini. Aidha, hatua
hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba,
2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa
kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika
Operesheni Tokomeza.
Utekelezaji
wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya
kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya
Maliasili na Utalii kuanzia sasa.
Aidha,
ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi
Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles
Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.
Hali
kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi
Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu
Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Vilevile,
Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo,
Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi
Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji –
Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori
katika Wizara ya Maliasili na Utafiti.
Nawaagiza
kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na
Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza
viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators)
nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo. Viashiria hivi ni hatua ya
kufanikisha yafuatavyo, 1) Malengo ya wizara, 2) Uwajibikaji, 3)
Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku. Ni sharti
tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima
natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.
Kwa
mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro
Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa
kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na
kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Baraza hili liwe
limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.
Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji,
utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.
Mungu ibariki Tanzania.
Asante.
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014
No comments:
Post a Comment