Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kimeanza kutoa fomu za uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga,
mkoani Iringa huku kikijinadi kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo
utakaofanyika Machi 16.
Uchaguzi huo unafanyika ili kujaza
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dk William
Mgimwa aliyefariki dunia Januari Mosi, mwaka huu Hospitali ya Kloof
Medi-Clinic nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu ya figo.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni
wa Chadema, Kigaila Benson alisema fomu zimenza kutolewa kuanza
Februari 5 na kazi hiyo itasitishwa Februari 9, saa 10:00 jioni.
Benson alisema upigaji kura za maoni
utafanyika Februari 10 mwaka huu, siku itakayofuata Kamati ya Utendaji
ya Jimbo itapitia maoni yaliyotolewa na kura za maoni kisha itapeleka
Kamati Kuu ya Chama yenye jukumu la kumteua mgombea.
"Febriari 12 mwaka huu, Kamati Kuu
itakutana na siku hiyo tutamtangaza mtu ambaye atapeperusha bendera ya
chama chetu, siku tutakayozindua kampeni na bajeti nzima itakayotumika,"
alisema. Chanzo: mwananchi
No comments:
Post a Comment