Kampuni
ya vifaa vya michezo ya nchini Marekani Nike imeungana na klabu za ligi
kuu nchini Brazil za Corinthians, Internacional, Santos, Coritiba na
Bahia kutengeneza jezi za njano kwa kila klabu ili kuonesha sapoti yao
kwa timu ya taifa ambayo itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka huu.
Jezi hizo
ni za pekee ambazo zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa rangi za klabu
husika na rangi ya njano ambayo ni rangi ya jezi za timu ya taifa ya
Brazil ambayo imeshinda Kombe la Dunia mara tano.
Ndani ya
jezi hizo kuna maneno yanayosomeka 'Nascido pra jogar Futebol' ambayo
yana maana 'born to play football.' Maneno hayo pia yanapatikana katika
jezi za timu ya taifa ambayo yamewekwa tangu mwaka 2010.
Umoja: Klabu za Corinthians, Internacional, Santos, Coritiba na Bahia watakuwa na jezi za tatu kuisupport Brazil
No comments:
Post a Comment