ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Thursday, February 6, 2014

TALIBAN WAJIGAMBA NA MBWA WA MAREKANI

Mbwa aliyekamatwa alikuwa anatumiwa 'na kikosi maalum cha jeshi la Marekani nchini Afghanistan
Kundi la wapiganaji wa Taleban limesema kuwa limemkamata Mbwa kutoka kwa wanajeshi wa Marekani Mashariki mwa Afghanistan.
Picha waliyoiweka kwenye akaunti yao ya Twitter, inaonyesha Mbwa mdogo wa hudhurungi akiwa na kamba ndogo shingoni.
Taliban wanasema kuwa Mbwa huyo kwa jina, 'Kanali' alikamatwa usiku wakati wa msako uliofanywa mwezi Disemba.
Mbwa huyo alikuwa na tochi ndogo, kamera na kifaa cha GPS.
Pia walionyesha silaha walizonasa wakati wa msako huo, ambazo hutumiwa na kikosi maalum cha jeshi la Marekani.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kumekuwa na taarifa za kiongozi wa Taliban katika eneo hilo kuonekana akiwa na Mbwa huyo ambaye sasa ni mfungwa wa kivita.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...