Naibu katibu mkuu wa CCM, Bara, Mwigulu Nchemba akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ifunda kwenye uwanja wa chuo cha Ifunda katika kampeni hizo.
Naibu katibu mkuu wa CCM, Bara, Mwigulu Nchemba akiwa amemshika mkono Bw. Godfrey Mgimwa ambaye anaiwakilisha CCM kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga.
Mwigulu Nchemba akitoa mazungumzo mbele ya umati wa wajumbe wa CCM pamoja na wakazi wa kijiji cha Ifunda katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo la Kalenga.
katibu mkuu huyo wa CCM, bara, akinena jambo na mgombea huyo kupitia tiketi ya CCM, Bw.Godfrey Mgimwa katika uwanja wa chuo cha Ifunda.
Mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Kalenga kupitia tiketi ya CCM, Bw. Godfrey Mgimwa akiwasilimia wajumbe wa CCM na wakazi wa kijiji cha Ifunda waliohudhuria mkutano huo.
Wajumbe wa CCM, wakiwa wamembeba Bw. Godfrey Mgimwa katika moja ya matukio yaliyoshuhudiwa leo kwenye uwanja huo wa chuo cha Ifunda.
Bw. Godfrey Mgimwa akitoa salamu zake kwa wajumbe wa CCM na wakazi wa kijiji cha Ifunda walio hudhuria na kumlaki katika mkutano huo wa kampeni za CCM.
uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 16, Machi, 2014. hivyo, CCM itawakilishwa na Bw. Godfrey Mgimwa ambaye anawania nafasi hiyo ya ubunge wa jimbo la Kalenga.
No comments:
Post a Comment