Na Kizitto Noya, Mwananchi
- Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makundi hayo ni yale yanayomsaidia aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambao wametajwa kutaka kuwania nafasi hiyo.
Dodoma. Kadiri siku
zinavyosogelea uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, ndivyo
mpasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unavyozidi, kutokana na
kuwapo kwa makundi mawili yanayojipanga kusimamisha wagombea na ambayo
yameanza kuendesha kampeni kuchafuana.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makundi
hayo ni yale yanayomsaidia aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Andrew Chenge na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambao wametajwa
kutaka kuwania nafasi hiyo.
Hata hivyo, wakati Chenge akiwa hayuko tayari
kuthibitisha nia yake hiyo, Sitta hakupatikana jana kuzungumzia suala
hilo. Lakini habari zinasema vigogo hao wameshajipanga kwa ajili ya mbio
hizo za uchaguzi na sasa wanatafuta watu wa kuwasaidia.
Makundi hayo yalianza wakati wa kikao cha ndani
cha CCM kilichofanyika mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais
Jakaya Kikwete, ambako habari zilisema, baada ya chama kumteua Pandu
Ameir Kificho kuwania nafasi ya mwenyekiti wa muda wa Bunge la Katiba,
mmoja wa wajumbe wa kikao hicho walimpendekeza Chenge kuwa mwenyekiti wa
kudumu wa bunge hilo.
“Hapo ndipo mgogoro ulipoanza. Kwanza tulimkubali
Kificho ili kupunguza wingu la ushindani kwenye uchaguzi wa mwenyekiti
wa kudumu. Lakini wajumbe tulimkataa Chenge kwa hoja nzito na mwenyekiti
alikubali na kuamua kuwa watu wakagombee bungeni.”
Tuhuma dhidi ya Chenge
Baadhi ya wabunge wa CCM wamesema ni ukweli ulio
wazi kwamba Sitta na Chenge ndio wanaofaa kuwania nafasi hiyo, lakini
mchuano utakuwa mkali kutokana na kila mmoja kuwa na ushawishi wa aina
yake kwa wajumbe ambao ndio watakaopiga kura kumchagua mwenyekiti.
“Wakati wa kuapa, wajumbe watatakiwa kushika
Biblia au Qur’an. Ila tusema ukweli, unawezaje kufanya kiapo cha utii
mbele ya mwenyekiti ambaye uadilifu wake unatia shaka? Alihoji mmoja wa
wajumbe wanaomuungano mkono Sitta.
Mjumbe mwingine alisema Chenge hazuiwi kugombea,
lakini ajiandae kujibu maswali makuu matatu, moja likihoji uadilifu wake
wakati kuna mikataba mingi ya wawekezaji kwenye kampuni za madini
iliyoshuhudiwa na yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni mibovu.
“Pia tutamtaka aeleze kwa nini alikubali Uenyekiti
wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri kwa uteuzi wa Spika, wakati
kanuni zinasema wenyeviti wachaguliwe na wabunge wenyewe,” alisema
mjumbe huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake.
Kauli ya Chenge
Chenge mwenyewe amepuuza tuhuma hizo akisema kuwa ni za watu wasiopenda kuelewa.
No comments:
Post a Comment