Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Kashillilah (katikati ) akiongea na Waandishi wa Habari.
Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashillilah,
amewaambia waandishi wa habari kuwa Bunge Maalumu la Katiba
litazinduliwa rasmi Februari 26, 2014 huku kila mjumbe akilipwa posho ya
shilingi laki tatu na siyo shilingi laki saba kama ilivyochapishwa
katika baadhi ya vyombo vya habari.
“Sisi
tumesikia kuwa Wabunge wa Bunge la Katiba wanalipwa 700,000 na wala
hatujui hili limetoka wapi, kwanza mamlaka ya kuidhibisha posho ni la
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hajaidhinisha Sh. 700,000.
Alisema
Wajumbe watalipwa posho ya kawaida ya Serikali ya siku (hakuitaja),
lakini alisema kutawakuwa na kodi maalumu ambayo itahusisha posho ya
kikao, usafiri, malipo kwa madereva na mengineyo. Hivyo posho ya kawaida
itakuwa Sh 80,000/=
No comments:
Post a Comment