Baada
ya uchunguzi wa muda mrefu kuitafuta ndege ambayo ilidhaniwa kuwa
imepotea au kupatwa na matatizo mengine baada ya kushindwa kufika sehemu
iliyotakiwa kwa wakati, taarifa za uchunguzi mpya zilizotangazwa na
waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak, imefahamika ndege hii Malaysia
Airlines ilidondoka kusini mwa bahari ya hindi.
Kutokana na uchunguzi wa ziada uliofanyika na data zilizopatikana
kutoka kwa shirika la Uingereza linalojihusisha na uchunguzi wa ajali,
sasa hivi hakuna matumaini ya kupona kwa abiria yeyote kwenye ndege
hiyo.

Ndugu wa abiria ambao walikuwa Beijing kusubiri ndege hiyo wanasema
wametumiwa meseji na shirika hilo ikisema ndugu zao wote wamefariki
kwenye hiyo ajali.
Waziri mkuu huyo Najib Razak hakuelezea zaidi kwa undani juu ya ajali
hiyo lakini kingine ambacho alikisema ni kwamba ndege hii ilianguka
katikati ya bahari na hakukua na ardhi yoyote ya karibu ambayo ingeweza
kutua.
No comments:
Post a Comment