Milipuko
mitatu katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi imesababisha vifo vya watu 6
na karibu darzeni mbili kujeruhiwa jumatatu usiku katika mtaa mkubwa
wenye wakazi wengi wa asili ya Kisomali wa Eastleigh.
Mkuu
wa polisi wa County ya Nairobi Benson Kibue anasema milipuko hiyo
ilitokea takriban saa moja na nusu usiku na kwa karibu wakati mmoja
katika migahawa ya Sheraton Café na The New Kwa muzairua Grill.
Kufuatana
na mmiliki wa Sheraton Café Bw. Patrick Gakuyu watu walikuwa wanatizama
taarifa ya habari ya saa moja kwenye televisheni wakati aliposikia
milipuko miwili na umeme kuzimika na kuwa katika kiza. Anasema anadhani
ni grunetti mbili zilizorushwa ndani ya mgahawa wake.
Jumapili
usiku karibu na mtaa huo mtu anayedhaniwa ni gaidi aliuwawa alipokuwa
anatengeneza milipuko yake pamoja na wenzake watatu. Na gruneti moja
ilipatikana siku hiyo hiyo ya jumapili katika mji wa pwani wa Lamu ndani
ya kanisa moja.
No comments:
Post a Comment