Agness Jerad Musaa.
Kibano!
Wanawake wawili, wakazi wa jijini Dar wamekumbwa na bonge la msala
baada ya kutiwa mbaroni na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti na
kupambana na madawa ya kulevya ‘unga’ ambapo wamekamatwa na mzigo huo
wenye thamani ya mamilioni ya shilingi, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Taarifa
zilizodakwa na gazeti hili kutoka ndani ya jeshi la polisi na
kuthibitishwa na kamanda wa kudhibiti madawa hayo nchini, SACP Godfrey
Nzowa zilidai kwamba wanawake hao walikamatwa na madawa hayo kwa nyakati
tofauti katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini
Dar hivi karibuni.
Pamela Kihanira.
Kamanda
Nzowa alipozungumza na gazeti hili aliwataja waliokamatwa kuwa ni Agnes
Jerald Mussa (42), mkazi wa Magomeni-Mapipa, Dar na Pamela Kihanira
Kibaya (33) (pichani)w, mwenye maskani yake Mbezi-Mwisho, Dar
Pamela na Agness wakiwa chini ya ulinzi mkali wa makamanda wa Jeshi la Polisi ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.
Kamanda Nzowa
aliweka wazi kwamba Agnes mwenye hati ya kusafiria (passport) namba AB
624446 ya Februari, 2014, alikamatwa Machi 30, mwaka huu, mishale saa
8:30 usiku akijiandaa kupanda ndege kuelekea nchini Uturuki na alikutwa
na kilo 1.2 za Cocain zenye thamani ya Sh. milioni 61.5.
Alisema
kwamba Pamela mwenye passport namba AB 516016 ya Aprili 12, 2012, yeye
alikamatwa Machi 31, mwaka huu, saa 8.00 usiku akiwa na kilo 3.5 za
Cocain zenye thamani ya Sh. milioni 179.7 akitokea nchini Brazil.
Kamanda
Nzowa aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wa kuwafichua wahalifu hao
na amewataka waendelee kutoa ushirikiano kama huo ili kudhibiti biashara
hiyo haramu.
Habari
za uhakika zilisema kuwa baada ya kuhojiwa na polisi, wanawake hao
walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 2, mwaka huu
ambapo kesi ya Agnes ipo chini ya Hakimu Geni Dudu wakati Pamela ipo kwa
Binge Mashabala.Kesi hizo zilitajwa kusikilizwa tena Aprili 16, mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment