Hakuna
mchezaji yoyote aliyefukuzwa kwenye timu baada ya kupoteza mchezo dhidi
ya Mgambo Shooting mwishoni mwa wiki, taarifa hizo zinasambazwa kwa
Propaganda ili kuweza kuvunja umoja uliopo ndani ya timu kwa wachezaji
na walimu pia kwa Viongozi na wanachama.Uongozi
wa klabu ya Young Africans unasikitishwa na taarifa zinazotolewa na
baadhi ya Vyombo Vya Habari tangu siku ya jumatano kwamba wachezaji Juma
Kaseja, Kelvin Yondani, Athuman Idd "Chuji" wamefukuzwa kwenye timu na
Emmanuel Okwi ameondoka kurejea kwao nchini Uganda ni za uongo mtupu.
Kelvin
Yondani hakuungana na wenzake kambini baada ya kuomba kupumzika na
kutatua matatizo yake ya kifamilia, Benchi la Ufundi walimpa ruhusa hiyo
kwa kuzingatia mchezaji mwenyewe asingeweza kutumika kwa mchezo wa
jumapili dhidi ya JKT Ruvu kufuatia kuwa na kadi tatu za njano,
ataungana na wenzake mara baada ya tu ya mchezo huuo.
Athumani
Idd "Chuji", David Luhende pamoja na kiungo Haruna Niyonzima ni
wagonjwa, wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanakua fit na kuungana na
wachezaji wao mara baada ya mchezo wa siku ya jumapili.
Juma
Kaseja yupo kambini pamoja na mlinda mlango Deo Munish "Dida" aliyekua
majeruhi kwa takribani wiki tatu kufuatia kupata jeraha katika mkono
wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Emmauel
Okwi yupo jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu kufuatia
kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo mwishoni mwa wiki, awali
Okwi aliiumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje na machela.
Okwi
akiongea na katibu mkuu wa Yanga Beno Njovu leo ofisini makao makuu ya
Klabu ya Ynaga, amesema anaendelea vizuri na ataaungana na wenzake mara
baada ya mchezo wa jumapili, lakini akisikitishwa na habari zilizotolewa
juu yake amabazo hazina ukweli wowote.
Kufuatia
wachezaji hao kushindwa kuungana na timu siku ya jumanne katika mazoezi
ya jioni, kocha mkuu Hans Van der Pluijm alichagua wachezaji 20 ambao
wap kambini kujiandaa na mchezo huo:
Magolikipa: Juma Kaseja, Deo Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barhez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Raja Zahir ,Oscar Joshua na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Frank Domayo, Said Dilunga, Nizar Khalfani , Salum Telela na Hamis Thabit
Washambuliaji: Hussein Javu, Hamisi Kizza, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu.
Waati
huo huo klabu ya Yanga imewasilisha barua ya malalamiko kwa TFF juu ya
mchezaji Mohamed Hussein Neto kuchezea timu ya Mgambo JKT pasipokuwa na
uhamisho wa kimataifa ITC, kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini,
mchezaji huyo ni raia wa Kongo na jina lake halisi ni Noel Melondoo.
No comments:
Post a Comment