Stori: Waandishi Wetu
ADAM Philip
Kuambiana amezikwa jana kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam huku akiacha maswali magumu matano kuhusu maisha, mazingira na
hatimaye kifo chake, Risasi Mchanganyiko linakupa moja kwa moja.
Marehemu
Kuambiana alifariki dunia Jumamosi iliyopita asubuhi akikimbizwa kwenye
Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
matibabu baada ya kuugua tumbo ghafla.
MANENO KUTOKA KWENYE MIDOMO YA WATU
Baada
ya kifo chake, maneno kutoka kwenye vinywa vya watu yalionesha ni
maswali magumu ambayo majibu yake yangepatikana kama marehemu angekuwa
hai.
Hata
hivyo, Risasi Mchanganyiko lilifanya kazi ya ziada kuhakikisha maswali
hayo yanapata majibu kwa ndugu au watu wa karibu na marehemu.
MASWALI MAGUMU MATANO
Maswali
ya watu kuhusu marehemu Kuambiana yako matano ambayo baadhi ya wasomaji
walitoa ombi kwa Magazeti Pendwa ya Global kuyafanyia kazi na kutoa
majibu yake kwa vile uwezo huo kwa Global upo.
SWALI LA KWANZA
Inadaiwa
kuwa asubuhi ya kifo chake, marehemu na wasanii wenzake walikuwa
kambini, Sinza jijini Dar. Wasanii hao walimgongea mlango kwa sababu
walitakiwa kwenda kurekodi filamu wakakuta mlango uko wazi, wakaingia.
Mke wa marehemu Janeth Rithe ambaye ni Diwani Kata ya Kunduchi (Chadema), akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.
Je, ni kwa nini marehemu aliacha mlango wazi wakati kuna maelezo kwamba alikuwa akilala na vifaa vingine vya kufanyia kazi?
Stara Thomas ambaye amewahi kuwa mchumba wa marehemu, anajibu hili:
“Ninavyojua
mimi Kuambiana alikuwa anavuta sana sigara. Mara nyingi akitaka kuvuta
alikuwa akitoka nje. Sasa huenda alfajiri ya siku hiyo alifungua mlango
akatoka kuvuta aliporudi hakuufunga tena.”
SWALI LA PILI
Yapo
madai kwamba, siku hiyo marehemu alikuwa na fedha nyingi. Hilo linaweza
kuthibitishwa na rafiki wa karibu wa marehemu ambaye alisema kuwa,
Ijumaa, yaani siku moja kabla ya kifo, Kuambiana alikuwa na fedha
nyingi.
Davina
akibebwa baada ya kuzidiwa wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Adam
Kuambiana kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar.
Kuhalalisha
hilo, hata mhasibu wa Gesti ya Silvarado, Sinza jijini Dar ambayo
marehemu na wasanii wake waliitumia kupiga kambi kwa ajili ya kurekodia
filamu alisema walikuwa wakimdai shilingi milioni mbili na siku hiyo ya
Ijumaa alilipa keshi.
Swali
ni je! Kama marahemu alikuwa na fedha nyingi japokuwa hakijajulikana
kiasi, baada ya kifo chake zilichukuliwa na nani na ameziweka wapi?
NDUGU WA MAREHEMU ANAJIBU
Ndugu
wa marehemu ambaye alisema si msemaji wa familia na akaomba jina lake
lisitajwe, alisema anachojua yeye marehemu hakukutwa na hata senti tano
mfukoni.
“Hilo
la kusema alikuwa na fedha siku hiyo hata sisi tunasikia tu. Lakini
sisi kama familia tunajua hakukutwa na pesa licha ya kwamba tumesikia
alikuwa akiwapa ofa watu kwenye mabaa. Kuna mtu nasikia alitoweka nazo,
tunamsaka kila kona.”
SWALI LA TATU
Wengi
wanatatizwa na makazi ya marehemu kwamba mtu angetaka kumpata Kuambiana
angekwenda wapi maana mara nyingi alikuwa akionekana kwenye baa
mbalimbali za jijini Dar hasa maeneo ya Sinza.
“Mimi
nimewahi kusikia kwamba, Kuambiana alikuwa hana makazi. Alipokutana na
Stara Thomas ndiyo akawa anaishi kwake, walipomwagana ikawa mwendo ni
uleule.
“Nimewahi
kusikia kuwa alipokuwa akipewa tenda ya filamu ndiyo makazi yake
yalikuwa kambini. Lakini sina hakina sana makazi yake japokuwa na mimi
ni msanii wa filamu kama alivyokuwa yeye,” alisema mwigizaji mmoja
akiomba asindikwe gazetini.
STARA ATAJA MIKOCHENI
Risasi Mchanganyiko lilizungumza tena na Stara ambaye alijibu:
“Mimi aliniambia makazi yake yalikuwa Mikocheni (Dar) lakini sikuwahi kufika. Lakini ninavyojua ni Mikocheni.”
Akizungumza
na gazeti hili msibani kwa mke wa marehemu, Bunju jijini Dar, ndugu
mmoja alisema anavyojua yeye marehemu alikuwa akiishi Bunju B.
SWALI LA NNE
Baadhi
ya mastaa walisikika wakisema baada ya kuachana na Stara, marehemu
alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa filamu anayeitwa Lulu
Jumanne ‘Selina’ Lakini swali likawa je, ni kweli?
RISASI LAMSAKA, LAMPATA SELINA
“Ni
kweli mimi na Kuambiana tulikuwa wapenzi. Baada ya kuachana na mke wake
wa ndoa (Janeth) alikuja kwangu tukaishi wote, lakini baadaye
tukaachana, nikasikia yuko na Stara.
“Hata hivyo walikorofishana na kurudi tena kwangu,” alisema Selina ambaye ndiye mpenzi wa marehemu hadi kifo chake.
SWALI LA TANO
Swali
la tano ni kuhusu filamu aliyokuwa akiishuti marehemu ambayo kaiacha
katikati inayoitwa Jojo. Marehemu alisema ni yake lakini kuna madai
kwamba, Stara Thomas naye anadai ni ya kwake.
Risasi Mchanganyiko lilimsaka Stara juzi kuhusu madai hayo ambapo alisema:
“Mimi
sina tatizo, kama marehemu alisema ni yake sawa tu. Ila ilikuwa ya
kwetu sote. Hata ikijulikana ni yake sidhani kama ni tatizo.”
AZIKWA
Marehemu
Kuambiana alizikwa jana katika Makaburi ya Kinondoni, Dar ikitanguliwa
na misa iliyosomwa katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambapo
aliagwa.
Mastaa kibao walifurika viwanjani hapo lakini wengi waliishiwa nguvu, kuanguka na kupoteza fahamu.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya shujaa Kuambiana – Amina.
Imeaandaliwa na Shani Ramadhani, Mayasa Mariwata, Deogratius Mongella, Hamida
No comments:
Post a Comment