Southampton
wanaamini bei waliyotaja ni haki kwasababu mchezaji huyo amekulia
katika akademi yao na wanatamani kukamilisha dili hilo kabla ya mchezaji
huyo kujiunga na kikosi cha Hodgson kitakachoweka kambi nchini Ureno
kuanzia mei 19.
Hodgson
kesho jumatatu atataja kikosi chake cha wachezaji 23 na wengine 7 wa
ziada kwa ajili ya kombe la dunia mwezi ujao nchini Brazil na Lallana ni
miongi mwa viungo watakaojumuishwa.
Kutokana
na idadi nzuri ya magoli ya kufunga na kufungwa, , Kikosi cha Manuel
Pellegrini kinahitaji pointi moja tu leo ili kutwaa ubingwa wa pili
ndani ya misimu mitatu.
Liverpool wanawaombea Man City wapoteze mechi na wao washinde iki kuweza kuchukua ubingwa.
Kumsajili
Lallana ni moja ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha kikosi cha
Liverpool kuelekea msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya UEFA.
Mmiliki
wa Liverpool, John W Henry amemuahidi paundi milioni 60, Brendan
Rodgers kwa ajili ya usajili jumlisha pesa atakazopata katika mauzo ya
wachezaji.
No comments:
Post a Comment