Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji
amesema kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio
mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya
kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye
msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akiongea na waandishi
wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa
kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi
lakini sasa amerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka kwa
Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji
wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza
mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.
Pamoja na kuondoka
kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga
inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa,
Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua
akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.
Aidha Manji amelifuta
rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani
ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya
Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku
pia wakishindwa kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi
sita, waliofutwa uanachama ni:
1. Ally Kamtande, 2.
Isiaka Dude, 3. Hamisi Matandula, 4.Waziri Jitu Ramadhani, 5.Mohamed Kigali Ndimba
, 6. Selaman Hassan Migali
Mkutano mkuu wa
mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa
Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze
kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai.
Suala la ujenzi wa Uwanja
wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni
majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es
salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na mda si mrefu.
No comments:
Post a Comment