ADV

ADV

ADVERTISEMENT CORNER

HUDUMA YA KUKATA TICKET ZA NDEGE ONLINE


SOMA HABARI

SOMA HABARI

Friday, May 9, 2014

MKE WA RAIS WA MAREKANI ‘MICHELLE OBAMA’ AUNGA MKONO KAMPENI YA #BRINGBACKOURGIRLS


Kampeni ya #bringBackOurGirls imeonekena kugusa hisia za watu wengi hali iliyopelekea kuungwa mkono na watu mbalimbali mashuhuri hasa wale wanaojua uchungu wa mwana akiwemo mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama, pamoja na wanamuziki kama vile LudaCris, John Legend, Naomi Campbell, Jamie Foxy,  Drake, Justine TimberLake, Alicia Keys, 2Face na wengine kibao.
Kwa huzuni kabisa,  mastaa waliotajwa hapo juu waliweza kuweka ujumbe kwenye akaunti na kurasa wanazomiliki za kwenye mitandao ya kijamii wakitaka kuachiliwa huru kwa wanafunzi wa kike 234 wa shule ya bweni ya Chibok ambao waliotekwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram yapata wiki mbili zilizopita katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
”Our prayers are with the missing Nigerian girls and their families. It’s time to .” aliandika mke wa Rais wa sasa wa marekani Bi.Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter .
Michelle ObamaMichelle Obama
Alicia KeysAlicia Keys
Justin TimberlakeJustin TimberLake
Drake
2Face Idibia
Real Men Don't Buy GirlMastaa mbalimbali  wakiwa na mbango yaliyobeba ujumbe mzito wa ”Real Men Don’t Buy Girls” ikiwa ni katika kupinga kitendo  kinachofanywa na Boko Haram cha kuwashikilia wasichana hao na kutaka kuwauza kwa watu wa mataifa mengine .

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...