Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha maombolezo
alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania
Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za
mwisho kwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy
Gomile-Chidyaonga leo katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia na maafisa wa
ubalozi wa Malawi alipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa Balozi wa
Malawi nchini Tanzania Marehemu Flossy Gomile-Chidyaonga leo katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, Balozi Frossie Chiyaonga, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini
Dar es Salaam, leo Mei 12, 2014. Mwili huo unatarajia kusafirishwa
kuelekea Malawi kwa maziko.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu,
Flossie Chidyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania,
aliyefariki ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga
mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam, jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji baadhi ya wanandugu na familia ya aliyekuwa Balozi wa
Malawi nchini Tanzania, Balozi Flossie Chidyaonga, wakati wa shughuli za
kuaga mwili wa marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam, jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Malawi wakati wa
shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania.
Sehemu ya waombolezaji waliojitokeza kwenye shughuli hiyo ya kuagwa mwili wa marehemu.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa
heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Flossie
Chidyaonga, aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania, aliyefariki
ghafla Ijumaa ya wiki iliyopita, wakati wa shughuli za kuaga mwili wa
marehemu zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es
Salaam, jana
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akitoa
salamu za rambirambi, wakati wa shughuli hiyo.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi
Haji Makame, akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili
kuhudhuria misa maalum ya kumwombea aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini,
Mh Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi
Haji Makame akibadilishana mawazo na Balozi wa Nigeria nchini Tanzania
Dk Ishaya Samaila Majanbu (kushoto).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu
Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule na
kulakiwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akisubiri kwenda kutia saini kitabu cha maombolezo kabla ya kuanza
kwa ibada maalum ukumbini hapo. Kushoto ni Makamu Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akisaini kwa huzuni Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha
aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga
kilichotokea Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei
2014. Kulia ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Balozi
wa Finland Tanzania, Sikka Antila wakilia kwa uchugu pamoja na Kaimu
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole wakati
wa misa maalum ya kumwombea aliyekuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania
Mh. Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), akisalimiana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole. Katikati ni Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila.
Kaimu
Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole
(mwenye mtandio mweupe) akibadilishana mawazo na baadhi ya Mabalozi
wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania nje ya ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Jeneza
lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie
Gomile Chidyaonga ukiingizwa kwenye ukumbi tayari kuanza kwa ibada
maalum na kutoa heshima za mwisho.
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Balozi wa Malawi nchini Tanzania Flossie Gomile Chidyaonga.
Mchungaji akiongoza ibada maalum ya kumwombea marehemu Flossie Gomile Chidyaonga.
Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bi. Tonia Kandiero
(kushoto) akiwa na baadhi ya mabalozi pamoja na wakuu wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa Tanzania wakati wa ibada maalum ya kumwombea marehemu
Flossi Chidyaonga iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Nyuso za simanzi zikiwa zimetawala ukumbini hapo.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhuria ibada msiba wa Balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard K. Membe (Mb)
akiwa mwenye huzuni kubwa kwenye misa ya kumwombea marehemu Balozi
Flossie Chidyaonga.
Familia ya karibu ya marehemu ikiongozwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini, Mh. Chisiza (kulia).
Huzuni, simanzi na majonzi vilitawala ukumbini hapo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akitoa mkono wa pole kwa ndugu wa karibu wa familia ya marehemu
mara baada ya kutoa heshima za mwisho.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa mkono wa pole familia ya balozi Flossie Gomile Chidyaonga.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mkono wa pole
kwa wafiwa.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero, akitoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga, akishindwa kujizuia wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Mh. Filiberto Sebregondi, akitoa heshima zake za mwisho.
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi .Joyce Mends-Cole, akitoa pole kwa wafiwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu,(wa tatu kulia)
, Balozi wa Zambia hapa nchini, Mhe. Judith Kangoma Kapijimpanga (wa
pili kulia) wakati wa misa maalum ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Balozi wa
Malawi hapa nchini Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga.
No comments:
Post a Comment