Kundi la Boko Haram limewaonesha wasichana wa Nigeria
linalowateka nyara wakiwa wamevalia hijab na kudai kuwa tayari wasichana
wote wamebadili dini na kuwa waislam.
Kundi hilo limetoa video ambayo imeoneshwa na shirika la Ufaransa
‘Agence France- Presse’ ambayo inaonekana ikiwa imechukuliwa porini
ikiwaonesha wasichana takribani 100.
Katika video hiyo yenye dakika 27, wanaonekana wasichana hao wakisema maneno mbalimbali yanayopatikana katika Quran.
“Msifuni Mungu, bwana wa dunia nzima.” Wasichana hao wanasema katika video hiyo.
Nae kiongozi wa kundi hilo, Abubakar Shekau ameeleza kuwa yuko tayari
kuwaachia wasichana hao kwa makubaliano ya kubadilishana na wafungwa wa
Boko Haram wanaoshikiliwa na serikali ya Nigeria.
Zaidi ya wasichana 270 wamepotea tangu kundi hilo lilipowateka nyara
April 14 mwaka huu huku wasichana wengine wakitoroka muda mfupi baada ya
kutekwa.
No comments:
Post a Comment