Kampuni
ya uwindaji ya Gree Miles Safari Limited(GMS) iliyokuwa ikifanya kazi
zake za uwindaji Tanzania ilifutiwa leseni yake rasmi wiki iliyopita
kutokana na kampuni hiyo kwenda kinyume na makubaliano na sheria za
uwindaji za Tanzania.
Ilifika
wakati ambapo kampuni hiyo ilithubutu kuwinda hadi ndege wakati
ilikuwa hajaruhusiwa ama kukubaliana na serekali ya Tanzania kufanya
hivyo.
Vibaya
zaidi kampuni hiyo ilianza hata kukamata wanyama wadogo na kuwachukua
wakati hilo pia halikuwa ndani ya makubaliano yake na serekali.
Hata
hivyo, baada ya waziri Nyalandu kuifutia leseni, kampuni hiyo
iliruhusiwa kufungua mashtaka mahakamani kutokana na hasara ambayo
itakuwa imesababishiwa ili sheria ichukue mkondo wake kama itaona kuwa
imeonewa kwa kitendo hicho.
Angalia
picha zake hapo chini ili upate kuona shughuli za kampuni hiyo kwa
ujumla pamoja uvunjifu wa sheria na makubaliano yake na serekali ya
Tanzania:
Kampuni hiyo ikiwinda ndege |
kampuni ya GMS ikiwa imekamata ndege |
Ikiwa imemkamata mnyama mdogo kwa lengo la kumbeba |
Ikiwa imemkamata mnyama kwa lengo la kuondoka naye |
Wawindaji wa GMS wakiwa wamemkamata ndege |
Hapa wawindaji wa GMS wanampakia mnyama waliokwisha kumuua kwenye gari |
Mnyama aliyejeruhiliwa kwa risasi. Anamaliziwa kwa risasi nyingine hapa chini: |
aliyekwisha kuuawa kwa risasi, tayari kuchukuliwa |
Wawindaji wakiwa mawindoni |
Wawindaki wakimpakia nyama waliyemuua |
Mnyama aliyeuawa, tayari kwa kusafirishwa |
Sasa
swali langu ni je, mpaka muda huu serekali inaposhtuka kuwa wawindaji
hawa wanavunja sheria ni kwa kiasi gani Tanzania imepata hasara kubwa?
Na
je, ina maana kuwa watanzania wameshindwa hata kuwa na makampuni ya
uwindaji mpaka kuyasajili makampuni ya wageni ambao hawana uchungu na
taifa letu?CHANZO BLOGU YA WANAINCHI