MWANAMKE ALIYECHOMWA MOTO SEHEMU ZA SIRI ASEMA HATORUDI KWA MUMEWE JAPO ANAUJAUZITO.
Agnes Marwa akiwa amelala kwenye kitanda katika kituo cha Afya Sungusungu
Agnes
Marwa (18 ) mkazi wa kijiji cha Mrito,Tarime Mara amesema kutokana na
ukatili aliofanyiwa na mumewe hayuko tayari kurudi kwa mwanamme huyo
ingawa ni mwaka mmoja sasa tangu waoane na kuwa na ujauzito wa mwezi
mmoja na nusu.
Marwa Chacha anatuhumiwa kumpiga,kumfunga kamba na kumweka nje wakati mvua inanyesha ,kisha akaenda jikoni
na kuchukua kijinga cha moto na kuanza kumuunguza sehemu zake za siri
baada ya kukuta shilingi 2000 kwenye pochi yake na kumtuhumu kuwa
amepewa fedha hizo na wanaume julai 13 mwaka huu.
Baada
ya kitendo hicho mtuhumiwa alitoroka na Agnes kwa mila za kikurya
alificha tukio hilo hadi julai 17 mwaka huu ndipo akapelekwa katika
kituo cha afya cha Sungusungu kilichopo Nyamongo.
Mganga
mfawidhi wa kituo cha afya Sungusungu Kagumilwa Kaijage amesema kuwa
siku aliyofikishwa kituoni hapo alikuwa na hali mbaya kwani alikuwa
akitokwa usaa katika sehemu zake za na mapajani kutokana na kuunguzwa
sehemu hizo.
Jeshi
la Polisi kanda maalum ya Rorya limesema mtuhumiwa pamoja na mama yake
wametoroka na hii ni baada ya kutoa taarifa,hata hivyo jeshi hilo bado
linaendelea kufanya utafiti ili liweze kumkamata mtuhumiwa.
jikoni na kuchukua kijinga cha moto na kuanza kumuunguza sehemu zake za siri baada ya kukuta shilingi 2000 kwenye pochi yake na kumtuhumu kuwa amepewa fedha hizo na wanaume julai 13 mwaka huu.