NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA HABARI,VIJANA,NA MICHEZO AZINDUA RASMI KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA"KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA
Mwina
Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina
Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza
Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na
Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu
hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la
Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo
isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Akijiandaa kukata utepe ili kuweza
kuzindua rasmi kitabu hicho cha historia ya Simba,Wanaoshuhudia kulia ni
mtunzi wa kitabu hicho Mwina Kaduguda akifuatiwa na Bwana Mkuki Bgoya
mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Ambao ndio wachapishaji wa kitabu hicho
Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota Bwana Mkuki Bgoya Akielezea namna walivyochapa kitabu hicho na ubora wake .
Mjumbe
wa kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Bwana Collin Frisch akiongea kwa
niaba ya Rais wa Simba,ambapo amempongeza sana Mwina Kaduguda na kusema
ameiweka Klabu ya Simba kwenye Kumbukumbu muhimu sana kwenye soka la
Tanzania hivyo inatakiwa aungwe mkono kwa nguvu zote.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia akitoa neno kumpongeza Mwina Kaduguda
kwa kufikiria mbali sana kwa kuweka soka la Tanzania kwenye maandishi
namna klabu ya simba ilivyoanza,Akaongeza kuwa Klabu za soka Tanzania
zinatakiwa kuwa na watu kama Mwina Kaduguda ili kuleta maendeleo ya
soka.Naibu waziri pia akasisitiza ni wakati wa kila mwanachama kujituma
kwa bidii na kuacha kukaaa kwenye korido za Klabu na kupiga Zoga.
Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi ya Kitabu ambayo ameomba apelekewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwina kaduguda Mtunzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" Akimkabidhi Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia Zawadi yake ya Kitabu.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji Klabu ya Simba Collin Frisch akiwa na Mtunzi wa
kitabu cha Historia ya Simba Mwina Kaduguda kwenye uzinduzi Rasmi wa
kitabu hicho kwenye ukumbi wa Klabu ya Simba
Wageni
waalikwa waliokuja Kushuhudia Uzinduzi wa Kitabu cha "HISTORIA YA
SIMBA" Kutoka kulia ni Fredrick Mwakalebela,Said Tulliy(Mjumbe wa kamati
ya Utendaji),Hassan Dalali(mwenyekiti Mstaafu) na Mtunzi wa kitabu
Hicho Mwina Kaduguda
Wapenzi,wanachama
wa Simba Pamoja na Vyombo vya habari waliohudhuria Uzinduzi wa Kitabu
cha "HISTORIA YA SIMBA" wakifuatilia kwa makini Uzinduzi huo
Hizo ni kopi za Kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" kilichozinduliwa leo na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia