

Baadhi
ya Mabaki ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za
utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET
usiku wa kuamkia leo.




Sehemu
ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina
la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la
kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo
na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo.Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko
la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai
Market kuteketea kwa moto.
Mulongo
ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka
hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto
na kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali
kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa
uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama
Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo
cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku
yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto
kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
No comments:
Post a Comment